|
|
Unaweza kupanga au kufuta historia yako ya simu, salamu za sauti, ujumbe wa sauti (sikizi na/au semi zote), Huduma ya Ujumbe Mfupi (SMS), na mazungumzo yaliyorekodiwa kupitia akaunti yako ya Google Voice. Ufutaji kama huo utaanza kutumika mara moja katika mwonekano wa akaunti yako, lakini kikasha chako, na historia ya simu zinazoweza kudaiwa zitabaki zikionekana kwenye akaunti yako. Mabaki ya nakala za data na akaunti zilizofutwa, isipokuwa maelezo ya rekodi ya simu, zinaweza kuchukua hadi siku 90 ili kufutwa kutoka kwenye seva zetu zinazotumika na zinaweza kubaki katika mifumo yetu ya hifadhi rudufu. Nakala zisizotambulika za maelezo ya rekodi ya simu, zisizokuwa na maelezo ya kibinafsi yanayoweza kumtambua mtu yatabaki katika mifumo yetu ili kufikia mahitaji yetu ya kuripoti na ukaguzi.
|