|
|
Unapopiga gumzo moja kwa moja katika Gmail au Google Talk, unaweza kuchagua gumzo lisirekodiwe ili chochote kitakachocharazwa kutoka wakati huo kisihifadhiwe katika akaunti ya Gmail ya mtu yeyote. Kufanya gumzo lisirekodiwe hutumika kwa watu binafsi, na hutumika kwenye gumzo zote. Hii inamaanisha kuwa mara unapochagua kutorekodi gumzo na mtu fulani, gumzo utakazopiga naye daima hazitarekodiwa, hata kama utafunga dirisha la gumzo na nyinyi wawili hamtapiga gumzo tena hadi baada ya miezi kadhaa. Hautahitaji kuchagua kutorekodi gumzo kila wakati unapopiga gumzo na mtu yule yule, lakini utahitaji kufanya uamuzi huu kwa kila mtu unayepiga gumzo naye.
|