|
|
Njia moja ambayo wahalifu wakati mwingine hufikia kompyuta yako ni kwa kutafuta matatizo yanayojulikana kwenye matoleo ya zamani ya programu zinazoendeshwa kwenye kifaa chako. Wanajua kuwa watu wengi kwa kawaida hawasasishi hadi matoleo ya sasa ya programu za kompyuta zao, ambayo yana ulinzi bora wa usalama. Google wanajua hili pia, ndio maana tulisanidi kivinjari cha Chrome kijisasishe otomatiki hadi toleo la sasa kila wakati unapokianzisha, ili uweze kupata ulinzi wa usalama bila kazi ya ziada.
|