|
|
Unaweza kugeuza kati ya Akaunti za Google kwa urahisi na haraka, kote kwenye eneo-kazi na kwenye simu ya mkononi. Kwa mfano, unaweza kuongeza Akaunti ya Google ya pili unapokuwa umeingia kwenye akaunti yako kuu na ubadilishe kutoka moja kwenda nyingine kati yao. Na kwenye kompyuta ndogo mpya za Google zenye hali za watumiaji wengi kama Nexus 7, ni rahisi kwa akaunti nyingi kuhusishwa na kifaa kimoja. Hii inawarahisishia watu tofauti katika familia yako kuangalia barua pepe zao au kufikia programu zao bila kuhitajika kuingia na kuondoka. Mara unapokuwa umefungua akaunti ya msingi, unaweza kuongeza akaunti kwa urahisi katika mipangilio ya kifaa.
|